Umuhimu wa Kliniki kwa Wajawazito
Kuhudhuria kliniki ya ujauzito mara kwa mara husaidia kufuatilia afya ya mama na mtoto.
Kliniki ya wajawazito (ANC) ni fursa muhimu ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na kubaini mapema changamoto zozote zinazoweza kujitokeza. Wataalamu wetu hufuatilia uzito, shinikizo la damu na hali ya jumla ya mama katika kila ziara.
Kuhudhuria kliniki mapema, tangu miezi ya kwanza ya ujauzito, huwezesha kupata chanjo muhimu, vidonge vya madini na ushauri wa lishe bora unaofaa kwa hatua husika ya ujauzito.
Katika Hanim Dispensary, huduma za kliniki ya wajawazito zinajumuisha ushauri wa afya ya mama, uchunguzi wa ultrasound na maandalizi ya kujifungua salama.
Panga Miadi Yako Leo
Jaza fomu hapa chini na tutakupokea kupitia WhatsApp ili kuthibitisha miadi yako haraka iwezekanavyo.
Weka Miadi